Sunday 8 March 2015

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: NANI KAMA MAMA?

Tunawapongeza wanawake wote popote walipo kwa mchango wao katika jamii,matunzo,malezi, ustahimilivu, busara zao na faraja zao. Kweli mwanamke ni kiumbe muhimu katika maisha. Nani kama mama?
Tuzidi kuwaheshimu kuwapenda kuwasaidia, na serikali nayo izidishe mapambano ya kuleta usawa wa kijinsia na kutambua kuwa mwanamke akiwezeshwa anaweza.
Mama huyu anafanya haya yote ili wanae waweze kupata kile anachoona ni chema katika maisha yao; Elimu kwanza.
Vai halisi na la kitamaduni la wanawake. Mwanamke khanga.
Baba huyu anaonyesha mfano wa kuigwa kwa wanaume wanaojua thamani ya mwanamke katika suala zima la kusaidiana majukumu ya kulea. Wanaume wengi huona aibu kuwasaidia wake zao au wanawake baadhi ya majukumu kutokana na mila potofu kwamba kazi hizi ni za wanawake. Haki sawa kwa wote ndio mpango mzima.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako