Thursday 12 March 2015

AJALI MBAYA YA BASI LA ABIRIA IRINGA

Inayosadikiwa kuwa ni orodha ya abiria waliokuwepo katika bus lililopata ajali.
Taarifa za awali kutoka jeshi la polisi mkoani Iringa zinaeleza kuwa basi la kampuni Majinja lenye usajili wa namba T438 CDE lililolaliwa na Lori lilikuwa limebeba jumla ya watu 49, idadi hiyo ni pamoja na dereva na kondakta wa basi hilo.wengi wa watu hao wamefariki dunia idadi ya majeruhi haijajulikana bado.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa kwenye mizigo mingi ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo kumepatikana madaftari mengi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam hivyo jeshi hilo linaendelea kufanya mawasoliano ma wamiliki wa gari hilo ili kujua kama lilikuwa limekodishwa kubeba wanafunzi wa chuo hicho ama ni mchanganyiko wa kawaida wa abiria.
Blog hii inaungana na watanzania wote kuomboleza msiba huu mkubwa. Tunawaombea waliofariki wapumzike kwa amani. Tunawaombea majeruhi wapate nafuu mapema na kurudi katik majukumu yao. Tunawapa pole wote walioguswa na ajali hii kwa msiba au majeruhi.
(Picha kwa hisani ya Iringa yetu Blog)

1 comment:

  1. Kwa kweli ni ajali kubwa sana ambayo imetokaa katika nchi yetu ya Tanzania. POLE SANA WALIONDOKEA NA FAMILIA ZAO . Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. AMINA.

    ReplyDelete

Maoni yako