Saturday 14 March 2015

KABLA YA KUANZA KULALAMIKA

Sie binadamu tumekuwa wakati mwingine twakosa shukrani kwa Mungu tukisema maisha magumu licha ya kwamba tunavyoishi ni vizuri tu ukilinganisha na wengine. Kuna watu wanalala nje,hawana nguo hawana chakula lakini bado wanamshukuru mungu wao kwa kuwaumba. Sie tatizo kidogo tu tutalalamika tutawalaani wazazi na hata kumkufuru Mungu
Mtazame mama huyu na mtoto wake. Makazi yao ni kwenye huu mfereji, na hapa mtoto anaandaliwa aende shule. Pengine mtoto huyu awapo shule anajitahidi kusoma sana tofauti na watoto wanaotoka katika mazingira mazuri. Kabla ya kulalamika shukuru.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako