Friday 13 March 2015

UVUMILIVU UNAPOFIKIA KIKOMO......


MKURUGENZI wa Jiji la Mwanza, Halifa Hassan Hida ameingia katika kashfa nzito baada ya mwanaharakati aliyefahamika kwa jina la John Masweta kutinga kwenye geti kuu la Makao Makuu ya Jiji la Mwanza jana huku akiwa amevaa gunia kumshinikiza mkurugenzi huyo amlipe shilingi 1,600,000 aliyopewa kama zawadi na uongozi wa mkoa na mkurugenzi huyo kushindwa kuilipa fedha hiyo kwa wakati.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kwenye lango kuu la kuingia ofisi za jiji hilo, Masweta alisema kuwa yeye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Environment & Conservation (TECO) aliyejitolea kwa zaidi ya miaka 20 kupanda miti na amekuwa akipewa tuzo mbalimbali kutokana na kazi hiyo na kuweza kuliokoa taifa katika majanga ya jangwa.
Mwanaharakati John Masweta akiwa kwenye geti kuu la Makao Makuu ya Jiji la Mwanza.
(Picha na maelezo kwa hisani ya Global Publishers)

No comments:

Post a Comment

Maoni yako