Monday 22 June 2009

TAARAB YAMPOTEZA NYOTA NASMA KHAMIS


Mwimbaji mahiri na aliyewahi kutamba sana kwenye anga ya muziki wa taarabu hapa nchini, Bibie Nasma Khamis wa Kidogo ( pichani) amefariki dunia usiku wa kumkia leo.
Baba mdogo wa Marehemu ambaye amejitambulisha kwa jina la Mzee Kaniki akizungumza na vyombo vya habari nyumbani kwake Kinondoni Sharif Shamba ambako ndiko msiba uliko amesema Marehemu alikuwa na matatizo ya shinikizo la damu tatizo lililokuwa likimsumbua mara nyingi, hata hivyo siku za hivi karibuni alishikwa na maralia na kupelekwa katika Hospitali ya Temeke ambako alilazwa na kukaa hapo kwa siku nne mpaka mauti yalipompata usiku wa kuamkia leo
Nasma Khamins atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi nzuri zilizokuwa zikipendwa na mashabiki wengi wa muziki kama vile "Naona mambo iko huku" wimbo uliovuma sana wakati huo akiwa na kundi la muungano kundi hilo likiwa hasimu mkubwa wa kundi lingine la la muziki wa Taarab TOT, ambapo mwimbaji mshindani wa Nasma alikuwa alikuwa Khadija Kopa.
Mungu ailaze mahali pema peponi Roho ya Marehemu Nasma Khamis Kidogo Amin

HABARI KWA HISANI YA www.michuzijr.blogspot.com na www.fullshangwe.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako