Sunday 28 June 2009

KILA MTU ATAUCHUKUA MZIGO WAKE MWENYEWE

Lakini jamani, hata kwa hawa????

2 comments:

  1. Tatizo ni kiasi. Nadhani ni vema kwa hawa kujifunza shughuli kama hizo, lakini WAFUNZWE na sio KUADHIBIWA. Wakibebeshwa kikuni kimojakimoja ama kukopo ka maji badala ya fungu zima la kuni na dumu la maji watajifunza. Hivi ni vitu ambavyo tunatakiwa kuwafunza. Wanatakiwa kujua ratiba ya maisha ya ndani na hata kuona mahangaiko na mkanganyiko wa maisha ambao wazazi wanapitia kuwafikisha walipo wao.
    Tatizo linakuja pale ambapo watoto wanatumika kama sehemu ya "nguvukazi" na kupangiwa mzigo sawa na mtu mzima na matokeo yake kwa kuwa hawawezi kuubeba kwa wakati mmoja, wanalazimika kurejea tena na tena na tena kubeba kidogokidogo na hapo wanaanza kuiona hiyo kama ADHABU badala ya ELIMU YA MAISHA.
    Kwa hiyo nadhani mzigo ukipungua na wao wakaoneshwa namna ya kufanya, watapenda na hilo ni la kusisitiza.
    Blessings

    ReplyDelete
  2. Ni kweli Mzee wa Changamoto. Asante kwa mchango wa mawazo.

    ReplyDelete

Maoni yako