Monday 1 June 2009

ALIYESALIMIKA WA MWISHO KWENYE MELI YA TITANIC AFARIKI DUNIA

Millvina Dean, wa mwisho kati ya waliosalimika kwenye tukio la kuzama kwa Meli kubwa ya TITANIC 1912, amefariki jumamosi hii huko Southapton-Uingereza akiwa na miaka 97.

Elizabeth Gladys Dean, aliyejulikana kwa jina la Millvina, alizaliwa February 2, 1912 na alikuwa na umri wa wiki 9 tu akiwa kwenye meli hiyo pamoja na wazazi wake Bertram Frank na Georgette Eva pia kaka yake mkubwa Bertram wakiwa wanaelekea Kansas.