Monday 1 June 2009

FAIDA ZA ZIWA VICTORIA KAHAMA NA SHINYANGA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Martha Philipo kutoka katika kijiji cha Iselamagazi, Shinyanga, mara baada ya kuteka maji na kumtwisha ndoo wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha kuchotea maji iliyofanyika kijijini hapo jana jioni. Kituo hicho ni moja kati ya vingi vya kuchotea maji vilivyo katika mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria hadi miji ya Kahama na Shinyanga. Kushoto ni Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya.