Monday 14 September 2015

SERIKALI YAJENGA CHUO CHA UNADHIMU NA UKAMANDA HUKO DULUTI ARUSHA

Muonekano wa baadhi ya majengo ya Chuo cha Unadhimu na ukamanda

Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akitoa ushauri wakati akikagua majengo ya Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu kilichopo eneo la Duluti nje kidogo ya mji wa Arusha leo. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda,kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange, Wapili kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Meja Jenerali Ezekiel Kyunga na kulia ni mwakilishi kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu Balozi Ibrahim Al Suweidy.umoja wa Falme za Kiarabu ulishirikiana na Serikali kufadhili ujenzi wa Chuo hicho.
Mkuu wa Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu Meja Jenerali Ezekiel Kyunga kulia akimuonyesha Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete maeneo mbalimbali ya Chuo hicho muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua Chuo hicho eneo la Duluti nje kidogo ya mji wa Arusha leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako