Monday 14 September 2015

DKT MAGUFULI AANZA KUONYESHA KUTOFAUTIANA WAZIWAZI NA MAFISADI. AMKAUSHIA MHE.CHENGE

Katika kile ambacho wachunguzi wa mambo ya
kisiasa wamekiita tukio la kimapinduzi na
mwanzo wa mabadiliko mapya ndani ya CCM,
Mgombea wa Urais kwa ticket ya CCM Dr. John
Magufuli
amefanya kile ambacho Rais Jakaya
Kikwete na Edward Lowassa wameshindwa,
kumtosa Andrew Chenge hadharani.
Mwanasheria huyo mkuu wa zamani ambaye
anahusika kwenye kashfa mbalimbali
zilizozikumba taifa hili, ambaye ndio alikuwa
mratibu wa kampeni za Urais za Edward Lowassa
alipokuwa CCM alijikuta kwenye wakati mgumu
leo pale ambapo Dr. Magufuli alipogoma
kumpandisha jukwaani na kumkabidhi ilani ya
CCM kama anavyofanya kwenye majimbo
mengine. Magufuli ambaye mpaka sasa ameweka
wazi adhma yake ya kuanzisha Mahakama ya
Mafisadi, inasemekana aliweka msimamo wake
wazi mbele ya Mwenyekiti wa kampeni za CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana kwamba hana
mpango wa kuwanadi wana CCM wowote ambao
wana kashfa za ufisadi, na amepewa baraka zote
za kukisafisha Chama cha Mapinduzi ili
kuonyesha tofauti na mgombea wa UKAWA
ambaye ana kashfa lukuki za ufisadi.
Tukio hili la leo linaelezewa na wachambuzi wa
Siasa kama mwanzo mzuri wa Magufuli
kujitofautisha na makada wa CCM wasio wasafi
na kurejesha imani ya Watanzania kwamba yeye
ndio atakayeleta mabadiliko bora zaidi kwa
Wananchi.
Itambuliwe pia, Dr. Magufuli amefanya kazi katika
awamu zote mbili za Rais Mkapa na Kikwete na
hajapata kashfa yoyote, tofauti na mgombea wa
Andrew Chenge

UKAWA ambaye kwa kipindi cha miaka 40
aliyokuwa ndani ya CCM amepata kashfa lukuki
ikiwemo ya Richmond, Ranchi za serikali, na kwa
sasa kuna sintofahamu kubwa kuhusu kauli zake
za kuomba kura- kanisani na hali yake ya kiafya.
Kwa sasa Dr. Magufuli amefaulu kizingiti hiki
kikubwa cha Mheshimiwa Chenge, na kugoma
kwake kumnadi kunatuma ujumbe kwa wale
mafisadi wote wa ndani na nje ya chama
kujipanga kwani anaonekana ana nia ya dhati
kusafisha Chama na Serikali ili kuwapa
Watanzania mabadiliko chanya wanayoyahitaji.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako