Thursday 14 May 2015

WATOTO CHINI YA MIAKA 5 KUPEWA CHETI CHA KUZALIWA BURE

Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhi cheki kwa mzazi wa mtoto
SERIKALI imeondoa ada ya cheti cha kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ikiwa ni hatua ya kuhakikisha kuwa kila kila mwananchi anapata usajili wa Vizazi nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa leo na Naibu wa Katiba na Sheria Ummy mwalimu wakati akizindua mkakati wa usajili wa Vizazi kwa watoto wa chiniya umri wa miaka mitano (U5BRI) mkoani Mwanza.

Mpango huo umelenga kumsajili na kumpatia cheti kila mtoto katika eneo la karibu na mahali tukio lilipotokea kwemye jamii kwa wakati muafaka kadiri inavyowezekana ukiratibiwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini nchini (RITA) ikiwa ni utekelezaji wa haki ya msingi ya mtoto kutambuliwa

No comments:

Post a Comment

Maoni yako