Thursday 7 May 2015

TASAF YAWAJIA JUU BAADHI YA WANAUME SINGIDA

Mwenyekiti wa kijiji cha Mwanga tarafa ya Nduguti wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida, Jackson Mkoma, akifungua mkutano wa tathmini ya matumizi ya fedha za TASAF awamu ya nne uliofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya kituo cha kilimo cha kijiji hicho.
Na Nathaniel Limu, Mkalama
BAADHI ya wanaume wa kijiji cha Mwanga tarafa ya Nduguti wilaya ya Mkalama mkoani Singida, wametuhumiwa kuwanyang’anya wake zao fedha za mradi wa kunusuru kaya maskini sana zinazotolewa na TASAF,na kuzitumia kunywea pombe, kitendo kilichodaiwa kukwamisha malengo na madhumini ya maradi huo.
Hayo yamesemwa na walengwa wa mradi huo awamu ya nne katika kijiji hicho,waliohudhuria mkutano ulioitishwa kwa ajili ya kufanya tathimini ya matumizi ya fedha zilizotolewa na TASAF kwa kaya masikini sana hivi karibuni

No comments:

Post a Comment

Maoni yako