Monday 11 May 2015

MVUA HIZI NA TAFRANI KATIKA FAMILIA

BABA:- Halloo mke wangu.. yaani ni shida sitaweza kurudi nyumbani, daraja limevunjika na kutoka Morogoro kurudi Dar haiwezekani
MAMA:- Mume wangu Morogoro ulienda bila kuniaga! ?
BABA:- Ilikuwa ni ghafla sana mke wangu sikuweza kukwambia
MAMA:- kha! Sasa watoto nani atawaangalia
BABA:- Unasemaje! We uko wapi kwani?
MAMA:- Niko Bagamoyo na daraja limeondolewa na maji sitaweza kurudi.
BABA:- Unasemaje we mwanamke.. nakwambia nikukute nyumban ndani ya dk 15
Baada ya dk 15 Baba kafika nyumbani.
MAMA:- Haya umefikaje kutoka Morogoro?
BABA:- Nimepewa lift na helikopta ya Mbowe!
(Picha hizi ni vielelezo tu hazihusiani na uhalisia wa maneno hayo)

No comments:

Post a Comment

Maoni yako