Thursday 7 May 2015

MVUA ZA MASIKA NA ADHA ZAKE

Mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini zimekuwa na manufaa kwa wengine, huku wengi wa wananchi hasa Jijini Dar es Salaam wakikumbwa na adha nyingi. Usafiri umekuwa wa tabu, barabara zinapitika kwa shida na shughuli mbalimbali zimesimama. Tazama picha hizi ujionee mwenyewe.
Hata kama ulikuwa ushikwi mkono basi kipindi hiki cha mafuriko kushikana mkono muhimu ili kuvuka salama.
Hii ingetokea kipindi cha ukoloni tungeita UTUMWA. Sasa ona mvua inatuletea nini tena hapa.
Watu wengi wamelazimika kutembea kwa miguu kwenda kwenye majukumu yao
Daraja la Kivule hali mbaya kwa mvua hizi
Hali Tete

No comments:

Post a Comment

Maoni yako