Monday 11 May 2015

TUNATARAJIA VIONGOZI WATAKAOTUTOA HUKU...

Wananchi wengi wa Tanzania bado wanaishi katika mazingira magumu sana. Kuna matabaka kati ya walio nacho na wasionacho. Hali hii imepelekea wengine kuishi maisha mazuri sana na wengine kuishi bila kuijua kesho yao itakuwa vipi. Pamoja na jitihada kubwa za viongozi wengi walio madarakani kwa sasa katika ngazi mbalimbali, bado hitaji la kuwatoa walio wengi kutoka katika umaskini linahitaji nguvu zaidi.
Tunawashukuru na kuwapongeza wale wote kutokana na kidogo walichojaliwa wanawasaidia wahitaji wa nchi yetu hii kama anavyoonyesha Mhe. Deo Filikunyombe Mbunge wa Ludewa kwa kutoa vifaa vya ujenzi na Kitanda cha kujifungulia wajawazito katika Jimbo lake la uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako