Monday 15 September 2014

TUWAPE WANAFUNZI MAZINGIRA BORA YA KUJIFUNZA

Ni Jumatatu ambapo wanafunzi wanaanza wiki ya pilika pilika za kutafuta elimu . Lakini nina uhakikwa kwa wanafunzi wa maendeo haya wanapofikiria taswira hizi hata hamu ya kwenda shuleni inapungua
Mwalimu amejikusanyia vitendea kazi vyake ila fimbo zimekuwa nyingi. Siui kama na vitabu ni vingi hivyo au pia kilichopo kichwani kwa ajili ya kuwagawia wanafunzi. Mbinu nzuri za ufundhishaji ndo zinasaidia na sio lundo la fimbo
Hapo ndo wamefika darasani. Kweli miaka 50 ya Uhuru bado wanafunzi wengine wanasomea sehemu kama hizi na hapo hapo twataka tupate viongozi wa taifa hili kesho. Kuna umuhimu wa kufanya kitu cha ziada.
Hivi watoto hawa wanaosomea chini ya Mbuyu huku watu waliochaguliwa kwenda kuwawakilisha kutengeneza katiba mpya hawaendi Bungeni na hivyo kukwamisha mchakato, watawaambia nn watoto hawa?

No comments:

Post a Comment

Maoni yako