Monday 8 September 2014

AJALI HIZI JAMANI. MUNGU TUEPUSHE

Basi la Kampuni ya DAR Express na Simba Mtoto leo yamepigana pasi huku Muheza Mkoani Tanga. Ajali hii haikuwa na madhara makubwa
Wakati majonzi ya ajali iliyotokea Musoma hayajapungua, Basi la kampuni ya AIRBUS limepata ajali maeneo ya Gairo. Basi hilo lilikuwa likitokea Jijini Dar kuelekea Tabora. Inasemekana watu 48 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa. Tunamwomba mungu azilaze roho zao peponi Amani. Tunawaombea na majeruhi wapate nafuu mapema
Tahadhari picha hii ifuatayo inahuzunisha sana

No comments:

Post a Comment

Maoni yako