Tuesday 1 July 2014

TIMU ILOKUWA IMEBAKIA YA AFRIKA KOMBE LA DUNIA IMETOLEWA

Mpira umeisha hivi karibuni na timu ya Algeria imetolewa kwa bao 2-1 dhidi ya Ujerumani. Katika pambano hilo ambalo lilidumu kwa dakika 120, Algeria ilipata bao la kufutia machozi katika dakika za nyongeza kabla ya mpira kumalizika. Kwa ushindi huu wa Ujerumani, Timu zote zilizokuwa zinacheza kombe la Dunia huko Brazil kutoka Afrika ndio zimeyaaga mashindano hayo. Jioni Nigeria ilifungwa na Ufaransa 2-0
Mchezaji wa Ujerumani Sami Khedira akimiliki mpira huku amebanwa na wachezaji wa Algeria

No comments:

Post a Comment

Maoni yako