Sunday 7 August 2016

MWANAMKE WA SHOKA "Joyce Kiria" ASEMAVYO

Mume wangu ni kiongozi...anayotaka kushiriki kuyafanya hayata-athiri tuu familia yake Bali hata Taifa letu... Mimi ni mdau wa maendeleo ya Wanawake na Watoto, sitakiwi kuongea nae haya mambo chumbani... Ni zaidi ya Binafsi... Sikatai madai yao Bali nakataa kata kata njia inayotumika kudai hayo madai ya msingi... UKUTA🚫🚫🚫🚫❌❌❌❌❌❌📌📌📌
.
.
Sihitaji ushauri wa baba, mama, mkwe, sheneji, mshenga, padre, mchungaji, shehe, marafiki, wanandugu, na wengine woooote unaowajua, sihitaji ushauri katika hili.... Nimeamua kusimama kuilinda kwanza NYUMBA yangu na pili TAIFA langu... Mnaonitukana jueni Sijaona Matusi mapya ya kunitingisha yote ni zilipendwa😂😂😂 ...
.
.
Tena mjue Sijipendekezi kwa chama chochote cha siasa kwa sasa, Bali nimejikita kufanya kazi nikishirikiana na Serikali iliyoko madarakani... Huu ni muda wangu wa kuchapa kazi na sibagui mtu kwa chama, kabila, rangi, ninashirikiana na kila mpenda maendeleo ya nchi kuleta maendeleo ya familia zetu.... Siasa labda 2020 panapo uhai.... Kwasasa ni KUPIGA KAZI TUU....
.
.
Manaoendelea na siasa naomba mtumie njia ambayo haitaligarimu Taifa letu jamani... Ebu niambie sasaivi kikinuka Mimi na familia yangu tutakimbilia wapi??? KUNA WENGINE WAMESHAWEKEZA HUKO NJE WANAZO SEHEMU ZA KWENDA KUJIFICHA... Haya Mimi na wanangu ntakwenda wapi???? Sidanganyikiiiiiii🙌🙌🙌
.
.
Tukubaliane kutokukubaliana kwamba, binafsi naona huu siyo wakati wa kujaribu kumkwamisha Rais kufanya kazi zake...Kama mlikubali akashinda mwacheni afanye kazi... Ni kweli Changamoto zipo katika nchi yetu lakini naomba zitumike njia bora zaidi za kutatua.... Na siyo UKUTA... period....
.
.
Naufunga mjadala huu naendelea kuchapa kazi... *MWANAMKE PIGA KAZI* (ntafuta post maana ujumbe ushafika). Bye✋✋✋

No comments:

Post a Comment

Maoni yako