Friday, 26 February 2016

MSAADA WA VIFAA-TIBA KUTOKA AZAM,PEPSI NA COCA COLA

Umoja wa Wazalishaji Vinywaji laini umetoa msaada wa vifaatiba vyenye thamani ya Sh Bilioni Kumi vilivyopokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Vifaatiba vilivyopokelewa jana ni pamoja na mashine za aina mbalimbali kama utra sound, mashine za kustulia moyo, vitanda vya watoto njiti, vitanda vya kujifungulia, vitanda 80 vya kawaida na magodoro yake, ambavyo viliwekwa kwenye makontena 20.

“Haijapata kutokea msaada mkubwa kama huu,” alisema Majaliwa kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye ghala la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) iliyoko Mabibo, Ubungo jijini Dar es Salaam.

“Natoa wito kwa makampuni mengine binafsi kuunga mkono jitihada za Serikali.”

Msaada huo wa vifaa tiba unawalenga zaidi watoto na wajawazito, ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kuboresha huduma za afya.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako