Tuesday 2 February 2016

HILI AU LILE?

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' amemshauri Mhe.Rais John Magufuli kuacha kujifungia Ikulu, badala yake apande ndege kwenda nje ya nchi ili akapate uzoefu wa masuala mbalimbali ya Uongozi. Wewe ungependelea Rais wetu afanye nini?

(A) Aendelee kutumbua majipu ikulu
(B) Apande ndege akajifunze ulaya?
Maoni ya wachache haya hapa;

1.Si hajui kiingereza ndio maana haendi nje anaogopa.
Mmesahau wakati wa kampen walikuwa anatafutwa na BBC World News akawakwepa. Atake asitake atakwenda tu nje, Tanzania hatuwezi tukaishi kama kisiwa!

2. Kwani ulaya kuna jinsi ya kufundisha kuongoza? Kama ndivyo basi Kikwete angekuwa raisi bora Tanzania na Afrika yote kwani muda mwingi aliutumia kusafiri na kuwa nje ya nchi. Acheni JPM afanye kazi, mbona wabongo kila kitu mnapenda kukosoa tu? Kwani haya anayofanya mmeona hayana tija kwa Taifa? basi jaribuni kuwa wavumilivu japo kidogo tuu ili tuone manufaa ya yeye kukaa Ikulu Tz na sio kusafiri kila siku.

3.Mbowe alisema "kuwa mpinzani sio kupinga au kukosoa kila jambo".Nakumbuka wakati kikwete akifanya ziara nje mara "raisi gani anapenda starehe za ulaya,magufuli kaja na style yake, mara "raisi gani anajifungia ikulu".Mnataka raisi wa aina gani Sugu?

4.Kukaa IKULU na hata kusafiri kila kitu kina umuhimu wake.... Itafika mahali lazima kama kiongozi wa nchi asafiri kwenda kwenye mikutano mikubwa au shughuli kubwa za maendeleo ya nchi.... Kubakia nyumbani tu kwa ajili ya kubana matumizi haileti maana

No comments:

Post a Comment

Maoni yako