Tuesday 23 February 2016

HAPPY BIRTHDAY H.E PRESIDENT MUGABE

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametimiza umri wa miaka 92 huku chama chake kikisema atawania tena urais 2018.
Mnadhimu wake mkuu alisema kiongozi huyo ambaye ameongoza nchi tangu mwaka 1980, bado ana uwezo kamili wa kuongoza Serikali licha ya tetesi kwamba hawezi kuongoza kutokana na umri.
Akizungumza na gazeti la Serikali Sunday Mail, Katibu Mkuu wa Rais Misheck Sibanda alisema tetesi hizo si za kweli na hazina msingi kwani Rais Mugabe ana ratiba ya wiki nzima kutekeleza kazi za Serikali na chama

No comments:

Post a Comment

Maoni yako