Saturday, 20 February 2016

MHE YOWERI MUSEVENI ATANGAZWA MSHINDI WA KITI CHA URAISI UGANDA

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi. Rais Museveni amepata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu. Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye amepata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako