Sunday 13 July 2014

MAAJABU YA MUNGU KOMBE LA DUNIA

Japo picha hii imetumika kama kielelezo tu, imetokea kwamba timu mbili zilizoingia Fainali Kombe la dunia na zinacheza leo ndio Mapapa wawili wa Kanisa Katoliki walikotoka. Papa Benedict XIV anatoka Ujerumani na Papa Fransis I anatoka Argentina.Bila shaka kila mmoja anaomba timu ya nchi yake ishinde, lakini kwa vyovyote mshindi ni mmoja na naamini wao ni viongozi wa Kanisa na sio wa mipira japo ushabiki wa mpira ni jambo tu la kibinadamu na sio dhambi.
Leo usiku Ujerumani inapambana na Argentina kuwania mshindi wa kombe la Dunia 2014, linalofanyikia huko Brazili. Mchezo huo utafanyika saa 4 usiku saa za Afrika Mashariki,katika Uwanja uitwao Estadio Maracana,Rio De Janeiro.
Mpaka sasa wafungaji Bora katika kombe hili la Dunia ni:
mabao Sita: James Rodriguez (Colombia)
Mabao Matano: Thomas Muller (Germany)
Mabao Manne: Neymar (Brazil), Lionel Messi (Argentina), Robin van Persie (Netherlands)
Mabao Matatu: Arjen Robben (Netherlands), Xherdan Shaqiri (Switzerland), Enner Valencia (Ecuador), Andre Schurrle (Germany), Karim Benzema (France)

No comments:

Post a Comment

Maoni yako