Wednesday 6 April 2016

ZIARA YA KWANZA YA MHE. RAIS MAGUFULI NJE YA TANZANIA TANGU AWE RAIS

Ziara hiyo ya Kwanza anaianya katika nchi ya Rwanda ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea Daraja la Rusumo linalounganisha nchi za Tanzania na Rwanda na pia kufungua kituo cha huduma mpakani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakifurahia mara baada ya kuzindua rasmi daraja hilo la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.
Muonekano wa sehemu ya Daraja hilo la Rusumo
Jiwe la msingi lililowekwa baada ya uzinduzi wa daraja hilo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako