RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein leo Jumamosi, April 9, 2016 ametangaza Baraza la Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali kwa kipindi cha uongozi wake wake kwa mujibu wa sheria.
Dkt. Shein amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo kutoka wizara 16 hadi kuwa wizara 13, ambapo wizara tatu amezivunja na kuzigawa ndani ya hizo wizara 13 za sasa. Mawaziri ni 13 na Manaibu waziri 7.
Ameongeza kuwa, mawaziri aliowatangaza leo atawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar.
==>Baraza la Mawaziri Zanzibar hao ni;
1). Ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi – Issa Haji Ussi Gavu.
2). Katiba na Sheria Utumishi wa Umma – Haroun Ali Sleiman.
3). Tawala za Mikoa na Idara maalum – Haji Omari Kheir.
4). Makamo wa 2 wa Rais – Mohamed Aboud.
5). Waziri wa Fedha na Mipango – Dk. Khalid Salum Mohamed.
6). Afya – Mahmoud Thabit Kombo.
7). Wizara ya Elimu – Riziki Pembe Juma.
8). Viwanda na Masoko – Amina Salum Ali.
9). Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Ali Karume.
10). Habari Utalii Utamaduni na Michezo – Rashid Ali Juma.
11). Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi – Hamad Rashid Mohamed.
12). Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mauldine Castiko.
13). Maji Ardhi Nishati na Mazingira – Salama Aboud Talib.
==>Pia amewataja manaibu waziri 7 kuwa ni:
1).Harusi Said Suleiman - Wizara ya Afya
2).Mmanga mjengo Mjawili – Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
3).Mahamed Ahmed Salum – Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi
4).Lulu Mshamu Khamis – Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
5).Chum Kombo Khamis – Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo
6).Juma Makungu Juma – Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira
7).Khamis Juma Maalim - Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.
Dkt Shein pia amewajumuisha Juma Ally Khatib na Said Sud Said kutoka vyama vya upinzani kuwa wajumbe katika baraza hilo
RMO MIRERANI AWATAKA WACHIMBAJI KUWEKA MATENKI YA MAJI
2 minutes ago
No comments:
Post a Comment
Maoni yako