Sunday 22 February 2015

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA

Ujumbe huu ungekuwa unamhusu binadamu ingefurahisha kuliko kuandikwa tu kwenye Daladala.Ni muhimu kusafisha maisha yetu kwa matendo mema ili Mungu azidi kutubariki na kufanya makazi pamoja nasi. Usidharau nafasi ya Mungu katika maisha yako mpendwa Mdau.

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Watanzania wasikilize na kufuata
mafundisho yanayotolewa na viongozi wa dini ili Tanzania iwe nchi
yenye watu waadilifu na wenye hofu ya Mungu.
Ametoa wito huo leo mchana (Ijumaa, Februari 20, 2015) wakati
akizungumza na maelfu ya waumini na wananchi waliohudhuria ibada ya
mazishi ya Askofu Mstaafu Magnus Mwalunyungu kwenye kanisa la Moyo
Mtakatifu wa Yesu la Tosamaganga, Jimbo Katoliki la Iringa.
“Leo ni siku ya pekee ya kuwasikiliza viongozi wa dini wakituasa
tujiandae kwa maisha baada ya kifo. Tukio hili la leo litupe nguvu ya
kukubali kwamba kifo kipo licha ya kuwa hakizoeleki na kinapotokea
kinaleta simanzi kubwa,” alisema.

1 comment:

Maoni yako