Thursday 26 February 2015

KWA WATUMIAJI WA USAFIRI WA TRENI YA JIJINI DAR........

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kutangaza kusitishwa kwa muda huduma ya treni ya Jiji kuanzia leo Jumatano jioni Februari 25 hadi Jumatatgu Machi 02, 2015 itakapoanza tena.

Kwa mujibu wa taarifa ya Uongozi wa TRL iliotolewa jioni leo Februari 25, 2015 uamuzi wa kusitisha huduma hiyo umesababishwa na vichwa viwili vya treni hiyo kuharibika na kuhitaji matengenezo makubwa katika Karakana Kuu ya Morogoro .

Taarifa imefafanua kuwa kwa vile kimebaki kichwa kimoja huduma hiyo haiwezi kuendelea hadi vichwa hivyo viwili vitakapo maliza kukarabatiwa siku ya Jumamosi huko Morogoro.

Kwa kawaida treni ya Jiji hutumia vichwa viwili wakati inapotoa huduma kati ya stesheni za Ubungo Maziwa na Stesheni kuu ya Dar, wakati kile cha tatu huwa cha akiba endapo dharura itakipata kichwa kimoja wapo wakati huduma inaendelea.

Aidha Uongozi wa TRL unawaomba radhi wateja wake na wananchi kwa jumla hasa wa eneo la Jiji waliokuwa wamezoeya kupata huduma hiyo kila siku kwa usumbufu utakajiotekeza .

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam,
Februari 25, 2015

*** (Picha na habari kwa hisani ya Michuzi Blog) ***

No comments:

Post a Comment

Maoni yako