Watu 17 wamepoteza maisha huku takribani 30 wakijeruhiwa baada ya watu wapatao watano wanaodaiwa kufunika nyuso zao kushambulia Chuo Kikuu cha Garrissa kilichopo Kaskazini mashariki mwa Kenya.
Shambulio hilo linadaiwa kufanyika mapema leo wakati waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa katika sala yao ya alfajiri.
Watu walioshuhudia tukio hilo wameeleza kuwa kuna majeruhi wengi ndani ya chuo hicho.
Wapiganaji hao wanadaiwa kuwa ndani ya chuo hicho mpaka sasa wakiwa wamewateka nyara watu kadhaa. Serikali ya Kenya kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi linafanya juhudi la kudhibiti tukio hilo.
Ramani ikionyesha eneo la tukio
RC GEITA AOMBWA KUINGILIA KATI MGOGORO WA MIRATHI
12 minutes ago
No comments:
Post a Comment
Maoni yako