Tuesday 6 May 2014

BUNGE LA BAJETI KUANZA LEO

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo linaanza kikao chake cha Bajeti, ambapo muda wa kuchangia na kuwasilisha bajeti za wizara mbalimbali, umepunguzwa.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel, alisema muda wa kuchangia Bajeti hiyo, umepunguzwa kutoka dakika 10 hadi saba na muda wa uwasilishaji wa bajeti za wizara mbalimbali, pia umepunguzwa.
Alisema kutokana na mabadiliko hayo, sasa kila wizara itapewa siku moja ya kuwasilisha bajeti yake na kujadiliwa. “Tumepima muda tukaona unatosha,“ alisema.
Mheshimiwa Mbunge mteule Ridhiwani Kikwete (Chalinze) akiwa mwenye furaha baada ya kutembelea Ukumbi wa Bunge ambapo anatarajiwa kuapishwa kuwa Mbunge rasmi na hivyo kushiriki katika Vikao hivi vitakavyoanza leo.
Pamoja na mambo mengine, magazeti ya leo yana habari hizi

No comments:

Post a Comment

Maoni yako