Thursday 7 April 2016

LEO NI "KARUME DAY"

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijiandaa kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muasisi ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar, ambapo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli ambae yupo ziarani nchini Rwanda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa pili kulia, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kulia na Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Dua ya pamoja mbele ya Kaburi la Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muasisi ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar,Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako