Friday 29 April 2016

JINSI YA KUUKARIBISHA NA KUUKUMBATIA UMASKINI

🏽
1. Kamwe usiamke mapema, endelea kulala na
kujinyosha mpaka pale njaa itakapokuuma.
2. Kamwe usipange jinsi ya kutumia pesa zako,
wewe zitumie tu pale unapozipata. Na zikiisha
kaa chini na jifikirie umezitumiaje.
3. Kamwe
usifikiri juu ya ku 'save' pesa zako, subiri mpaka
uwe nazo nyingi ndio uanze ku 'save', utasave
vipi pesa zako wakati unazo kidogo?
Wanaokuambia usevu pesa hawakutakii mema
katika matumizi yako.
4. Kamwe usijiingize katika biashara ambazo
huwa mnaziita 'za wasiosoma' wewe ni mhitimu
wa chuo kikuu ulie soma bhana utafanyaje
biashara ya viazi? Utauzaje duka? Utauzaje viatu
vya mitumba? Hizo ni biashara za wasioenda
shule. Wewe unapaswa ukae ofisini upigwe na
kiyoyozi.
5. Kamwe usifikiri kuanzisha biashara mpaka
pale Malaika atakaposhuka toka mbinguni
kukuletea mtaji wa kuanzia biashara.
Watakuambiaje uwekeze wakati hujapata hata
Milioni? Hata kama wafanyabiashara wengi kama
kina bakheresa walianza kuuza mgahawa, wewe
ni smart, unatakiwa uanze na mamilioni katika
biashara zako.
6. Lalamika kuhusu kila kitu,
isipokuwa usilalamike kuhusu uvivu wako na
attitude yako. Ilaumu serikali ya Magufuli,
zilaumu benki zilizogoma kukukopesha fedha,
zilaumu kampuni mbalimbali ambazo zimekutosa
kwenye ajira. Wote hao wana roho mbaya
hawataki kukufanya uwe tajiri!
7. Tumia pesa nyingi tofauti na unachokipata.
Kufanikisha hili nunua bidhaa za kutumia kwa
mkopo, azima pesa kwa washkaji nunua kitanda
cha Milioni moja, nunua Brand new LG flat
screen, pendezesha kwako. Kopa pesa benki
nunua Verossa, watoto wa mjini wakukome.
8. Shindana katika kuvaa. Hakikisha unavaa kila
aina ya fashion mpya ya nguo. Nunua kila aina
ya simu mpya inayotoka, kama ulinunua sumsung
galaxy S6 kwa milioni moja, uza hata laki sita
halaf ongezea hela ukanunue sumsung galaxy
S7. Zimetengenezwa kwa ajili yetu
bhana.Ukishindwa kununua gari mpya, nunua gari
ya mtumba ambayo gharama zake za
kulihudumia ni mara mbili ya mshahara
unaoupata, au gari linalokaa muda mrefu gereji
kuliko barabarani.
9.Wape wanao kila wanachokitaka kwa kuwa
wewe ni mzazi bora, hawatakiwi kuhangaika wala
kufundishwa utu na thamani ya pesa,
usiwafundishe juu ya kutunza na kuheshimu
fedha. Usiwafuatilie kabisa katika masomo yao.
Waache wakue wakiwa wavivu na waje kuwa
masikini kuhakikisha kuwa hawawezi kukusaidia
pale utakapozeeka.
10. Tembelea viwanja vyote vya bata, na uzuri
wamiliki wa maeneo ya starehe wanatujali yaani
wanafungua maeneo mapya kila siku, tembelea
yote. Kula bata kula bata, Nakwambiaje We
Kulaaa Bataa. Na ukishahakikisha kwamba
unatekeleza hayo yote, kaa chini na utafakari
kuwa siku zote fainali nzuri huchezwa uzeeni!
Ponda raha kufa kwaja!
UMASIKINI MWEMA.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako