Tuesday, 15 March 2016

VIJANA WAASWA KUFANYA KAZI NA SI KUCHEZA POOL NYAKATI ZA KAZI

Hayo Rais Magufuli ameyasema alipokuwa akiwaapisha Wakuu wa Mikoa

Rais John Magufuli leo amewaapisha wakuu wa mikoa wapya aliowateua hivi karibuni na katika hotuba yake amewataka wakuu wa mikoa hao wapya kuhakikisha vijana wanafanya kazi na kuacha uzembe.

Rais Magufuli amewataka wakuu wa mikoa hao kuhakikisha hakuna vijana ambao watakuwa wanakwenda kucheza pool table asubuhi na badala yake vijana hao wanatakiwa kufanya kazi kweli kweli hata kwa kulazimishwa.

"Nimeamua kuwateua wakuu wa mikoa nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika mikoa yenu.

"Napenda niwape pole kwa sababu mtakwenda kufanya kazi kweli kweli kutatua kero za wananchi wetu.

"Lakini pia niwaombe wakuu wa mikoa mkasimamie watu wafanye kazi hasa vijana.

"Haiwezekani vijana leo hii unawakuta saa mbili asubuhi wanacheza Pool table wakati wakina mama wanalima shambani, kama hawataki kufanya kazi kwa kupenda walazimishwe kufanya kazi. Atakayekataa mpelekeni kambini akafanye kazi" amesema Rais Magufuli

No comments:

Post a Comment

Maoni yako