Wednesday 1 July 2015

SIMBA S.C YAZINDUA KADI YA UANACHANA YA KISASA

Afisa MtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu Wakiwa wameshika Mfano wa Kadi ya Club Hiyo waliyoizindua Leo.
Klabu ya Simba leo hii imeandika historia kwa kuzindua Kadi Mpya za Wanachama ambazo zinamwezesha kila Mwanachama wa Simba kupata bima ya maisha hadi Tsh 250,000 ikiwa atafiwa na mwenza au mtoto au yeye mwenyewe kupitia bima ya maisha iitwayo Simba Pamoja. Pia Simba leo hii imezindua Kadi za watoto yaani Simba Cubs.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako