Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Zuberi Kabwe usiku huu ametangaza rasmi Bungeni Dodoma kuachia kiti hicho alichokipata kupitia CHADEMA.
Mhe. Kabwe ametangaza kung'atuka nafasi hiyo baada ya Mwenyekiti wa Bunge Mhe Mussa Hassan Zungu Kumruhusu kutoa kauli binafsi mara baada ya wabunge kumaliza kupitia vifungu vya sheria ya Maafa ambayo hata hivyo haikupitishwa kwa kutotimia akidi ya wabunge ambao nusu yao hawakuwepo ukumbini.
Mhe Zungu alimtakia kila la heri Mbunge huyo machachari ambaye amesema ameamua kuachia ngazi baada ya chama chake kumfukuza. Hata hivyo alimalizia kwa kusema kwamba anategemea kuwa nao tena mwezi Novemba mwaka huu. Hakufafanua. Video ya tamko lake hilo inaandaliwa. Kaa chonjo...
Mhe Zito Kabwe akisoma barua aliyomwandikia Mhe.Spika wa Bunge kuhusu kung'atuka kwake Ubunge.
Mpenda nyumbani nimeamua kuungana nanyi kuwaletea blog hii maalum inayowapa habari za nyumbani Tanzania na habari toka sehemu mbalimbali lakini zenye lengo la kuelimisha,kukosoa,kupongeza na kuburudisha jamii. Karibuni Nyumbani!
No comments:
Post a Comment
Maoni yako