Tuesday 16 May 2017

MJUE RUBANI WA KWANZA MWANAMKE TANZANIA

Gayeti la Daily News la February 12, 1985 linaripoti, kuwa Mwanamama Elizabeth Olotu anaandika historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kurusha ndege. Amerusha kutoka Dar kwenda Mafia na kurudi. Bakari Mwapachu, Mkurugenzi Mkuu wa ATC aliyekuwa abiria kwenye ndege hiyo aina ya Twin Otter alikuwa na haya ya kusema;

" Betty ametua ardhini kwa namna bora ambayo sijapata kuishuhudia kabla!" ( Kutoka maktaba ya Kwanza Jamii na Mjengwablog)

Je, hali ikoje leo?
Mbali ya mwenzetu Cecylia Gellejah tuna marubani wangapi wanawake?

Yuko wapi Elizabeth Olotu?

No comments:

Post a Comment

Maoni yako