Thursday 9 January 2014

SERIKALI ITAZAME HILI:KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

Basi la kampuni ya Mtei Express T 742 ACU linalofanya safari zake kati ya Singida na Arusha leo limeteketea kwa moto baada ya wananchi wachache wa kijiji kimoja huko Singida kulichoma moto. Hii inafuatia ajali ya pikipiki Aina ya SkyGo T 368 BXZ ambapo basi hilo liligongana na pikipiki ilokuwa na abiria wanne na watatu kati yao ambao ni wa familia moja kufariki dunia. Akizungumzia tukio hilo la kusikitisha,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea leo saa moja na dakika moja asubuhi huko katika kitongoji cha Ijanuka kijiji cha Kisasida Mkoani Singida Ila ni budi wananchi kuacha tabia ya kujichukulia maamuzi bila kushirikisha vyombo vya dola. Pia Blog hii inawaasa wananchi wote kuwa makini hasa watumiapo vyombo vya moto au kuwepo barabarani.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako