Saturday 11 January 2014

DUNIANI KUNA MAMBO: 1. HUYU NDIE NABII HUKO BRAZIL ANAYEJIITA "YESU" 2. WAAMINI WAAMRIWA KULA MAJANI/NYASI

Inri Cristo, 66,  akiongea na wanafunzi (wafuasi) wake nje ya kanisa lake liliopo Brasilia nchini Brazil. INRI ni neno la kilatini lenye maana "Yesu Mnazareti,Mfalme wa Wayahudi" kama kibao kilichoweka juu ya msalaba wa Yesu kilivyosomeka nyakati zile. Na mchungaji mmoja huko Afrika Kusini katoa mpya akiwaamuru waumini wake kula majani/nyasi kama namna ya kumkaribisha Mungu maishani mwao. Mchungaji  Lesego Daniel wa Rabboni Centre Ministries katika mji wa  Pretoria nchini Afrika ya Kusini kawambia waumini watoke nje wale majani ili wawe karibu na Mungu. Ila sijui kama waumini hawa wameyasoma vizuri maneno ya Yesu mwenyewe kwenye biblia Mathayo 24:11 "Watatokea manabii wengi......"

No comments:

Post a Comment

Maoni yako