Friday 9 October 2015

MZEE KINGUNGE NGOMBARE MWIRU AWANADI UKAWA MKUTANO WA KAMPENI ARUSHA

Mwanasiasa Mkongwe Nchini, Mzee Kingunge Ngomale Mwiru, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Arusha wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Sinoni, Unga LTD, Jijini Arusha leo Oktoba 8, 2015.

KADA Mkongwe wa Chama cha Mapinduzi CCM,Kingunge Ngombale –Mwiru ambaye amekiaga chama hicho ,ameendelea kukitolewa lawama cha hicho kusema CCM pumzi yake imefikia mwisho na haikitaki kupewa tena dhamana ya kuongoza nchi

Akizungumza wakati wa Kampeni za kumnadi Mgombea Urais kupia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambaye anaungwa mkono na Vyama vya Ukawa,Edward lowassa zilizofanyika leo Arusha Mjini na kushuhudiwa na umati mkubwa wa watu ambao uliosababisha shughuli nyingi kusimama.

Ambapo Kingunge amedai chama chake hicho kilichomlea kimechoka na hakina nia ya kweli ya kumkomboa mtanzania kwa lindi kubwa la umasikini.
Amesema CCM anayoijua yeye tangu ilipokuwa TANU ilikuwa yenye misingi na kuweka mipango ya kumletea maendeleo moja kwa moja lakini amedai CCM hile sio hii ya sasa kwani hii ya sahivi imetekwa na watu wachache wenye kujali maslahi binafsi na sio kumleta maendeleo mtanzania.
Kingunge huku akishangiliwa kwa nguvu,ammshukia pia Rais Jakaya Kikwete kwa kusema utawala wake umeua uchumi wanchi,
“Leo uchumi wa nchi umeporomoka,wakati Mkapa anamwachia nchi Kikwete uchumi ulikuwa kwenye hali nzuli,lakini baada ya kuingia yeye uchumi wan chi umedorola huku umasikini unazidi kuwa mkubwa kwa watanzania’

No comments:

Post a Comment

Maoni yako