Friday 9 October 2015

MHE. MREMA WA TLP AMKUBALI MAGUFULI


Leo katika mkutano wa CCM katika jimbo la vunjo, akihutubia nyomi ya watu, mgombea urais wa CCM John Pombe Magufuli alimwombea kura mgombea wa TLP, Augustino Mrema kwa wakazi wa Vunjo kwamba wamchague kuwa mbunge wao huku mgombea wa CCM wa jimbo hilo Innocent Shirima akiwa pembeni yake akishangaa bila kuamini.

Magufuli alisema pia kwamba mrema akichaguliwa atamwingiza kwenye baraza lake ya mawaziri.

Wakati hayo yakijiri viwanja vya himo, Mrema alikuwa njia panda na wakati Magufuli amemaliza mkutano wake alipita na 'entourage' yake kuelekea Same.

Mrema alikuwa amesimama anaongea na watu hapo njia panda, msafara wa Magufuli ulimpita Mrema kuelekea Same, lakini baada ya dakika 10 convoy ya Magufuli ilirudi njia panda ili kumsalimia mrema, wakazi wa Vunjo walifurika na Magufuli alimwomba Mrema aongee kidogo. Mrema alimsifia Magufuli kwa barabara alizojenga katika jimbo la Vunjo.

Magufuli nae alirudia akisema mbatia hafai kuwa mbunge ila wamchague Mrema ambaye ni jembe na mchapakazi kama yeye na watu walilipuka kwa shagwe.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako