Saturday 10 October 2015

DKT. MAGUFULI ASIFIA KUGUNDULIWA KWA GESI BAGAMOYO

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema kugundulika kwa gesi ya Bagamoyo mkoani Pwani itasaidia kuimarisha uchumi na ujenzi wa viwanda nchini.

Hayo aliyasema jana wilayani Bagamoyo katika mikutano yake ya kampeni iliyofanyika katika majimbo ya Chalinze na Bagamoyo, ambapo alisema gesi hiyo itasaidia ujenzi wa viwanda katika serikali yake.

"Kwanza niwapongeze kwa kugundua gesi hapa Bagamoyo, tena imegunduliwa katika eneo la Ruvu. Na hii itakuwa na manufaa kwa uchumi wa Taifa na kwa wananchi wa Pwani kwa ujumla.

"Gesi hii itasaidia sana ujenzi wa viwanda vya kisasa katika serikali ya Magufuli ya awamu ya tano. Tutajenga viwanda na tutatoa ajira za uhakika kwa vijana wa nchi hii pamoja na Tanzania yote," alisema Dk. Magufuli

No comments:

Post a Comment

Maoni yako