Friday 16 October 2015

MWENYEKITI MWENZA UKAWA NDG.EMANUEL MAKAIDI AFARIKI DUNIA

Mwenyekiti wa NLD, ambaye ni mwenyekiti mwenza wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Dkt. Emmanuel Makaidi amefariki jana majira mchana katika hospitali ya Nangao mkoani Lindi.

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Dkt. Makaidi ambaye alikuwa mgombea ubunge katika jimbo la Masasi alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.
Dkt. Makaidi ni mgombea ubunge wa tano kufariki katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
Blog hii inawapa pole wafiwa wote na Mungu aipokee Roho ya marehemu.Amen

No comments:

Post a Comment

Maoni yako