Saturday 27 February 2016

MSIBA: MMILIKI WA MABASI YA NGORIKA "MBERESERO" AGONGWA NA GARI NA KUFARIKI

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Ngorika Bus service, yenye makao yake makuu Kisangara mkoani Kilimanjaro, bw. STEPHEN Mberesero amefariki dunia mjini hapa baada ya kugongwa na gari aina ya Land cruiser wakati akizungumza na simu.

Kamanda wa polisi wa MKOA wa Tanga Mihayo msikhera alisema Jana kuwa ajali iyo ilitokea juzi SAA 2;30 usiku katika Barbara kuu ya segera-njiapanda ya himo mjini Korogwe.

Alisema Mberesero ambae mabasi yake hufanya safari Kati ya mikoa ya Arusha,tanga,Daresalaam na singida,marehemu alikuwa amesimama pembeni ya kituo cha mafuta cha Lake oil na kugongwa na gari hilo.

Mfanyakazi wa kampuni hiyo ,Adam Miraji alisema bosi wake huyo alikwenda Korogwe kuangalia Kiwanja kwajili ya kununua kujenga kituo cha mafuta.

Kama unavyojua bosi wetu pamoja na kufanya biashara ya Mabasi,alikuwa anamiliki vituo mbalimbali vya mafuta mkoani Kilimanjaro,Dar es Salaam na Arusha,hivyo alipokuja Tanga alituambia anakwenda Korogwe kuangalia Kiwanja cha kujenga kituo kipya cha mafuta,alisema Adam.

Alisema bosi wake huyo alikuwa ameliweka gari lake katika kituo cha mafuta cha Lake oil na kwamba alishuka kwajili yakuelekea katika Kiwanja hicho.

Wengi waliokuwepo eneo la ajali hawakujua kama ni yeye hadi tulipokwenda kuchukua mwili wake ndipo wakashtuka,Alisema.

Kamanda Mihayo alisema wanamsaka Dereva aliyesababisha ajali hiyo kwa uzembe na kusababisha kifo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako