Tume ya uchaguzi ya Tanzania Bara (NEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji Damian Lubuva imemtangaza Rasmi mgombea Urais wa CCM, Dr John Pombe Magufuli kuwa mshindi halali wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya jumapili wiki iliyopita.
Kwa Mujibu wa jaji Lubuva, Dr magufuli amepata ushindi wa kura Milioni 8 ( 8,882,935 ) sawa na asilimia 58.45% huku akimwacha kwa mbali mpinzani wake wa karibu , Edward Lowassa (Chadema ) ambaye amepata jumla ya kura Milioni 6 ( 6,077,848 ) sawa na asilimia 39.97%
Dkt. Magufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu watakabidhiwa rasmi vyeti vya ushindi tar 30 Okt saa nne asubuhi katika ukumbi wa hoteli ya Diamond Jubilee
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii Oktoba 29, 2015
Mama Salma Kikwete akimpongeza rais mteule
wananchi wakishangilia ushindi wa dkt Magufuli
VIONGOZI WATAKIWA KUYASEMEA MEMA YALIYOFANYWA NA RAIS SAMIA
47 minutes ago
No comments:
Post a Comment
Maoni yako