Thursday 25 June 2015

WEMA SEPETU: "NAWEZA KUWA MBUNGE BORA"

Wema Sepetu ameeleza sababu 5 za yeye kuweza kuwa Mbunge bora kabisa baada ya kutangaza nia yake ya kutafuta nafasi hiyo ya uwakilishi kupitia CCM – Viti Maalum mkoani Singida. Zifuatazo ni sababu hizo 5:

1. Nina kipaji cha uongozi, kuanzia ngazi ya shule ya msingi, sekondari, chuoni, katika taji langu la Urembo na Majukumu kama Miss Tanzania na pia kama mfanyabiashara.

2. Niko karibu na wananchi wa rika zote, naelewa matatizo yao na nimekuwa tayari nikishiriki katika kuyatatua katika ngazi mbalimbali. Naweza kuwaleta watu pamoja.



3. Naamini katika dhana ya mwanamke anaweza, sio tu akiwezeshwa bali akiamua mwenyewe kwamba anaweza. Nia yangu ya kuwa Mbunge ni chachu kwa wasichana wengine kwamba wanaweza kufanya yale wanayotaka kwenye maisha na wakayafanya kwa ufanisi.



4. Mimi ni kijana na mbunifu pia. Shida nyingi za vijana kwa dunia ya leo zinahitaji ubunifu katika utatuzi. Mfano elimu ya ujasiriamali katika kupambana na ajira, afya ya uzazi katika kuweza kufanya shughuli zako vizuri, haki za wanawake ili waweze kushiriki katika kujenga nchi yetu, n.k. Nataka kupiga hatua zaidi katika kuchangia ubunifu wangu kutatua matatizo ya vijana katika uwanja mpana zaidi kwa kutumia ubunifu huo na exposure yangu ya ndani na nje ya nchi.



5. Naamini katika mabadiliko. Kwamba vijana lazima washiriki kujenga jamii wanayoitaka. Naona kuna mengi ambayo naweza kuchangia, mengi ambayo hayako sawa. Sioni sababu ya mimi kukaa pembeni na kusubiri mwingine abadili yale ninayotaka yabadilike wakati nina uwezo wa kufanya hivyo.

- See more at: http://patahabari.com/2015/06/24/wema-sepetu-sababu-5-kwa-nini-naweza-kuwa-mbunge-mzuri/#sthash.Hfb8rVIy.dpuf

No comments:

Post a Comment

Maoni yako