Tuesday 2 June 2015

RAIS WA FIFA JOSEPH SEPP BLATTER ATANGAZA KUJIUZULU

Rais wa FIFA Sepp Blatter ametangaza kujiuzulu wadhifa huo ikiwa ni siku nne tu baada ya kutangazwa kushika nafasi hiyo. Hata hivyo amesema kuwa ataendelea kushikilia nafasi hiyo hadi uchaguzi utakapofanyika tena. Uchaguzi huo unatarajiwa wakati wowote kati ya Dec 2015 na Machi 2016

“Nilijiskia mkamilifu kwa kugombea tena kwenye uchaguzi wa FIFA nikiamini kwamba kilikua ni kitu muhimu kwa FIFA. Uchaguzi umeisha lakini changamoto za FIFA hazijaisha.
Japokua nina madaraka kutoka kutoka kwa wanachamana wa FIFA, lakini sijiskii kama nina madaraka kutoka kwa dunia nzima ya wapenda soka, wachezaji na vilabu".

No comments:

Post a Comment

Maoni yako