Friday 17 October 2014

BUSARA YA LEO: MAMBO YA KUJITAHIDI KUFANYA KABLA YA KUFIKIA MIAKA 30

1. Tambua uwepo wa Mungu na jitahidi kuzingatia maadili ya imani yako.
2. Jifunze kuweka akiba ya fedha tena bila kuigusa aidha benki au taasisi za fedha
3. Tafuta mpenzi sahihi na tulia nae kupanga maisha
4. Ishi mahali pa peke yako, sio kukaa na washkaji au mashoga tu
5. Lipa madeni yako ya zamani yote. Pia watake radhi mliokosana, jenga amani na watu.
6. Jenga mwili wako na jitahidi kutunza afya yako.
7. Jitahidi kuwa na marafiki wanaokujenga na kukupa changamoto za kimaendeleo za maisha.
8. Anza kuweka vitega uchumi kama kununua ardhi, biashara n.k
9. Jitahidi kuvaa kwa heshima sio ili mradi tu. Kata K na vimini sio dili
10.Tambua na ukubali kuwa umekua na uache tabia za kitoto au kufuata mkumbo.
11.Yaache ya zamani yapite na uanze upya.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako