Tuesday, 10 November 2015

RAIS MAGUFULI AHUZUNISHWA NA HALI YA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya kumsikitisha.

“ Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini. Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko” Amesema Balozi Sefue
mhe Rais Magufuli akimtazama kwa huruma Mama akiwa na mtoto wake wakiwa sakafuni katika Hospital ya Muhimbili

No comments:

Post a Comment

Maoni yako