Wednesday 26 August 2009

NANI ALAUMIWE?

Wadau,leo ngoja niongelee tabia ya "KULALAMIKA" bila kuchunguza zaidi nani wa kulalamikiwa na nini sababu ya kulalamika.
Katika picha hizi mbili hapa chini:


Mama huyu mfanyabiashara wa khanga na vitenge,ameuchapa usingizi katika eneo la biashara yake. Si ajabu mwisho wa siku akifanya mahesabu ya mapato yake kwa siku ataanza kulalamika "oooh siku hizi wateja hakuna, biashara haichanganyi, Rais hatuangalii watu wake,viongozi wazembe, njaa sana,nchi ya tabu sana hii" na maneno mengine kama hayo. Lakini sidhani kama katika tathmini yake ya kufanya biashara alizingatia vigezo ya biashara. Kwa mfano,mazingira anapofanyia biashara pana mwelekeo wa kuvuta wateja?, kauli yake kwa wateja je?, bei za bidhaa?, aina za bidhaa na mengine kama hayo. Zaidi sasa tunapoangalia picha hii, ni ukweli kwamba sidhani kama wateja watavutwa kuja kununua kitu kwako wakati wewe umelala, muda utakaotumia kuamka, kujiweka sawa na kuanza kuhudumia mteje tayari atakuwa keshakereka. Tusibaki tunalaumu tu,tuangalie hayo.


Katika picha hii nayo tunamwona jamaa huyu,yaonekana nae ni mfanyabiashara au mfanyakazi katika gari. Yeye kaona sehemu ya kupumzikia ni chini ya gari, tena gari lenyewe laonekana halina break imara ndio maana wameweka jiwe karibu na tairi.Lakini kiutaalamu uzito/egemeo la gari na uzito/egemeo la hilo jiwe haviendani. Hapo atakuwa amelalamika weeeeee kwamba hali ya maisha ngumu hadi amepata usingizi. Kwa mfano kama ni gari la kubeba mchanga hata mteja akija na kukuta amelala hivyo ni vigumu sana kumwamsha maana mteja unapokuja unategemea upokelewe kwa shangwe na maneno ya mvuto,"Mteja ni Mfalme" Halafu pia kwa bahati mbaya likitokea la kutokea labda gari limebiringika,ndio kusema hapo lazima watu waandae nyimbo za maombolezo.

Haya na mengine mengi ni ya kuangalia badala ya kulalamika tu.
Picha kwa hisani ya www.samvande.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako