Tuesday 4 August 2009

KUDUMISHA MILA NA DESTURI

Ukitamka "Mbege", watu wanajua moja kwa moja unarejea "Wachagga". Ila wachagga wenyewe wanaitika leta hapaaaaaaa.
Naam, ndio hao hapo chini. Kuna wakati nilitembelea sehemu za Uru- Kilimanjaro kwa mwaliko, nilivutiwa na watu hawa kwa kuona wamefanya mabadiliko kidogo katika unywaji wa mbege, badala ya kutumia chubuku moja kwa wote, hapa kila mtu alikuwa na ya kwake, hii ni hatua nzuri kwa kuepuka viini tete vya kudhuru afya ambavyo vinaweza kusambaa kwa kutumia chubuku moja kwa wote. Kilichonivutia zaidi ni heshima wanayopewa watu wakubwa, yaani watoto kupewa mbege kabla ya wakubwa, hapana!

No comments:

Post a Comment

Maoni yako